7 wakamatwa kwa ujambazi Dar

Friday, February 26, 2010 / Posted by ishak /

JESHI la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam limefanikiwa kuwakamata watu saba wanaosadikiwa kuwa ni majambazi wa kutumia silaha katika eneo la Mbezi kwa Yusuph
Kamishna Msaidizi wa Polisi (ACP), Charles Kenyella, aliviuambia vyombo vya habari kuwa, jeshi hilo limewakamata watu hao kwa kupata taarifa kutoka kwa wasamaria wema ambapo waliwagundua wakati wakijiandaa kwenda kufanya uhalifu.

Alisema mara baada ya kupata tarifa hiyo askari waliwafatilia mara moja majambazi hao na kufanikiwa kuwaona ambapo walikuwa wakitembelea gari dogo aina ya Baloon wakielekea maeneo ya Mbezi.

Alisema kutokana na uzoefu wa askari hao walifanikiwa kuwatia mbaroni na katika pulukushani jambazi mmoja alitaka kutoroka lakini walifanikiwa kumkamata baada ya kumfyatuliwa risasi mguuni.

Alisema majambazi hao walikuwa na silaha zikiwemo mapanga, mabomu yaliyotengenezwa kienyeji, betri na vifaa maalumu vya kujikinga na mabomu.

Hivyo majambazi hayo yanaendelea kushikiliwa na polisi huku upelelezi ukiendelea.


source nifahamishe

0 comments:

Post a Comment