Mume Akutana na Mkewe Kwenye Taarabu, Amshushia Kipigo

Monday, February 22, 2010 / Posted by ishak /


Mwanaume mmoja jina halikuweza kupatikana mara moja, alianza kumpa kichapo cha nguvu mkewe baada ya kumkuta katika ukumbi wa starehe akijivinjari kwa kuwa hakutegemea kumkuta mahali hapo usiku huo.
Sakata hilo lilitokea mwishoni mwa wiki, majira ya usiku, katika ukumbi wa Travetine Magomeni wakati Jahazi Taarabu ilipokuwa ikifanya onyesho ukumbini hapo.

Mwanaume huyo alifika ukumbini hapo huku akijua kwamba mke wake hatakuwa mahali hapo kwa kuwa alidai alimuaga anakwenda kwenye harusi ya ndugu yake na wakati akipapasa macho huku na huko alimuona mke wake akicheza ukumbini humo.

Hivyo alimuacha aendelee na kucheza na mziki ulipoisha mke wake huyo alirudi kukaa kwenye kiti na mume huyo ndipo alipomfuata alipokaa na kumtaka atoke nje ya ukumbi waondoke nyumbani.

Mwanamke huyo kwa vile alipania kuhudhuria shoo hiyo alimjibu mume wake huyo hatoki ukumbini na amuache hadi atakaporidhika na kuamua kuondoka yeye mwenyewe.

Kutokana na majibu hayo ya mkewe, mume huyo alichukua uamuzi wa kuanza kumshambulia kwa kumkata vibao vya nguvu mkewe hali iliyofanya kuzuke zogo kubwa mahali hapo na mwanamke huyo kuendelea kung’ang’ania kwenye kiti akiashiria haondoki mahali hapo.

Hali hiyo ilizua mtafaruku mkubwa hali iliyofanya mabaunsa kuingilia kati sakata hilo.

Mwanamke huyo alizidi kuonyesha msimamo wake na kuwaambia mabaunsa kuwa haondoki kwa kuwa alilipia na mabaunsa kumtaka atoke nje ya ukumbi kwa kuwa mumewe alikuwa anafanya fujo ukumbini hapo.

Mwanamke huyo alipoonekana ni king’ang’anizi ilibidi mabaunsa wamnyanyue na kiti alichokalia ili amani irudi mahali hapo kwa wengine waliokaa mahali hapo.
mwanamke huyo alivyopakizwa kwenye gari ndogo na kuondoka huku wakirushiana maneno ya hapa na pale na mumewe huyo.
source nifahamishe

1 comments:

Comment by Ney on February 25, 2010 at 2:26 AM

Hapo inaonyesha ni upungufu wa outing katika familia hiyo iweje kila mtu aende kwa wakati wake, pia iweje mwanamke asingizie anaenda harusini na huku mwanamme anaenda sehemu hiyo hiyo alipoenda mkewe kwa nini wasingepanga tu kama wote wanapenda burudani ile wakaenda wote kwa amani?
Yaelekea huyo mama pia alichoshwa na kitendo cha kuwekwa ndani kama pazia alihitaji kutoka walau kufurahi nae.

Post a Comment