Watoto Watumiwa Kama Waganga na Wanajeshi wa Jamhuri ya Kongo

Saturday, February 27, 2010 / Posted by ishak /


Wanajeshi wa waasi wanaopambana na majeshi ya serikali katika jamhuri ya Kongo wanatuhumiwa kuwateka watoto wadogo na kuwatumia kama waganga.
Makundi ya kutetea haki za binadamu yamesema kuwa watoto wenye umri mdogo katika jamhuri ya Kongo wanatekwa na kutumiwa kama waganga kwenye maeneo ya vita ya mashariki mwa Jamhuri ya Kongo.

Katika ripoti ya makundi ya kutetea haki za binadamu iliyotolewa ijumaa, wanamgambo wa kundi la Mai Mai wamekuwa wakiwatumia watoto kama waganga kwa imani kuwa watoto kwakuwa wengi wao huwa hawajui na hawajihusishi na mambo ya mapenzi, huwa na nguvu kubwa za uchawi.

Katika ripoti hiyo Umoja wa mataifa umetakiwa kuwanyang'anya silaha wanamgambo wa Mai Mai na kuwaachia huru watoto wanaoshikilia mateka ambao wamegeuzwa kuwa waganga.

Mashariki mwa Kongo kumekuwa na vurugu tangia vita vya wenyewe kwa wenyewe vilipotokea nchini Rwanda mwaka 1994.

Kundi la Mai Mai ni mojawapo ya makundi mengi yaliyojikita mashariki mwa Kongo ambapo wapiganaji wake mara nyingi hutumia mishale na mapanga.


source nifahamishe

0 comments:

Post a Comment