Mtu Mwenye Nywele Ndefu Kuliko Wote Duniani Afariki

Saturday, February 27, 2010 / Posted by ishak /


Mwanaume wa nchini Vietnam aliyekuwa akitambulika kama mtu mwenye nywele ndefu kuliko watu duniani amefariki dunia huku nywele zake zikiwa na urefu wa mita 6.8.
Tran Van Hay aliingia kwenye kitabu cha rekodi za dunia mwaka 2004 wakati huo alikuwa na nywele zenye urefu wa mita 5.6 lakini hadi wakati anafariki juzi nywele zake zilikuwa na urefu wa mita 6.8.

Hay alianza kuzifuga nywele zake miaka 50 iliyopita kwakuwa alikuwa akiumwa sana kila alipokuwa akizikata nywele zake, gazeti moja la nchini Vietnam lilimnukuu mke wake, Nguyen Thi Hoa akisema.

Vyombo vya habari viliripoti kuwa Hay alikuwa akiishi maisha ya kawaida tu akifanya kazi ya kuuza dawa za mitishamba lakini siku zote nywele zake zilikuwa zikimzuia kufanya baadhi ya mambo.

Hakuna taksi ya pikipiki iliyokuwa tayari kumbeba Hay kwakuwa alikuwa hawezi kuvaa Helmet kutokana na ukubwa wa nywele zake.

Hay alipenda kuzikusanya nywele zake na kutengeneza kitu kama ndoo juu ya kichwa chake.

Hay alifariki juzi nyumbani kwake katika mji wa Kien Giang uliopo kusini mwa Vietnam.


source nifahamishe