Mwanamieleka wa Marekani Apigwa na Mkewe

Wednesday, February 24, 2010 / Posted by ishak /


Mwanamieleka maarufu wa Marekani Ric Flair amejuruhiwa baada ya kushambuliwa na mkewe nyumbani kwake.
Mwanamieleka maarufu wa Marekani, Ric Flair ilimbidi awaite polisi baada ya kushambuliwa na mkewe kwenye nyumba yao iliyopo North Carolina.

Katika taarifa aliyoitoa kuhusiana na tukio hilo, Ric Flair ambaye anajulikana sana kwa manjonjo yake ulingoni, alisema kuwa kutokuelewana na mkewe ndio sababu ya mtafaruku huo na kwamba yeye hakufanya kosa lolote.

Mamlaka husika zilisema kuwa polisi waliitwa kwenye nyumba ya Ric Flair ambapo Flair alilamika kuwa mkewe alikuwa akimshambulia.

Ric Flair alionekana akiwa na majeraha kutokana na kichapo hicho toka kwa mkewe lakini alikataa kupatiwa matibabu na watu wa ambulansi.

Polisi walimtia mbaroni mkewe wa Flair bi Jacqueline Beems mwenye umri wa miaka 41, walimtupa jela kwa muda na kumuachia huru masaa machache baadae.

Flair mwenye umri wa miaka 60 bado anaendeleza kucheza mieleka kupitia TNA baada ya kutumia miaka mingi sana ya kipaji chake chake cha mieleka kwenye WWE.

source nifahamishe