JESHI la Polisi Mkoa wa Mara tayari limefanikiwa kuwakamata watu kumi wanaohusishwa na mauaji ya kinyama ya watu 17 wa ukoo mmoja katika Manispaa ya Musoma yaliyotokea mwanzoni mwa wiki iliyopita na kuacha historia ya pekee mkoani humo.
Hadi kufikia jana mchana, jeshi la polisi nchini limefanikiwa kukamata watu 10 mkoani Mara wanaohusishwa na mauaji ya watu 17 wa ukoo mmoja.
Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Mara, Robert Boaz, amesema hadi sasa watu hao wameshakamatwa na msako mkali unaendelea ili kuhakikisha watu wote waliohusika katika kufanya unyama huo wanakamatwa na kufikishwa katika vyombo vya sheria.
Kamanda Boaz alisema watu hao walikamatwa katika maeneo tofauti ndani na nje ya mkoa huo baada ya kupata taarifa za uhakika kutoka kwa raia wema ambazo zimekuwa zikifanyiwa kazi na jeshi lake.
Pia amewataka wananchi kuzidi kutoa taarifa kwa siri kuhusiana na watu hao.
Amesema timu kubwa ya askari wake wamesambazwa kila kona ya mkoa wa Mara na nje ya mkoa ili kuwasaka watu hao wauaji na kusema kazi hiyo itafanikiwa kwa jeshi hilo.
Amesema utaratibu wa kisheria utakapokamilika watu hao wanatarajiwa kupandishwa mahakamani muda wowote kuanzia sasa.
source nifahamishe
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 comments:
Post a Comment