Sala Kuwafufua Wachungaji Waliofariki Kwa Ajali Kenya

Wednesday, February 24, 2010 / Posted by ishak /


Waumini wa kanisa la Pentekoste nchini Kenya wamegoma kuwazika wachungaji wawili waliofariki kwa ajali ya gari wiki moja iliyopita na waumini hao wamekuwa wakikesha wakisali wakiamini wachungaji hao watafufuka kama YESU.
Waumini wa kanisa moja la Pentekoste magharibi mwa Kenya wamegoma kuwazika wachungaji wawili wa kanisa hilo waliofariki kwa ajali ya gari wiki moja iliyopita na wamekuwa wakisali mbele ya majeneza yao muda wote wakiamini kuwa watafufuka kama alivyofufuka YESU.

Mchungaji Patrick Wanjohi na mchungaji Francis Kamau Ndekei, walifariki februari 15 mwaka huu kutokana na ajali mbaya ya gari lakini waumini wao wamekuwa wakiamini kuwa wachungaji hao wamelala tu na wala hawajafariki.

"Hatutawazika kamwe, kwakuwa hawajakamilisha misheni zao hapa duniani, tunawahitaji warudi duniani kumalizia majukumu yao kwani bila ya wao kanisa litakufa", alisema mmoja wa waumini hao.

Awali uongozi wa kanisa hilo ulisema kuwa wachungaji hao watafufuka siku ya jumamosi na kuwafanya maelfu ya watu washinde kwenye mvua kubwa sana wakisubiria wachungaji wao wafufuke. Hata hivyo siku ya jumamosi ilimalizika bila wachungaji hao kufufuka.

Mamia ya waumini bado wanaendelea kusali masaa yote mbele ya majeneza ya wachungaji hao wakisubiria miujiza ijitokeze na wachungaji hao wafufuke.

source nifahamishe