Video ya Ngono Yamfikisha Mahakamani 50 Cent

Saturday, February 27, 2010 / Posted by ishak /


Nyota wa muziki wa Hip Hop wa Marekani 50 Cent amefunguliwa kesi mahakamani kutokana na video ya ngono ya mwanamke mmoja wa nchini humo ambayo 50 Cent ameiweka kwenye tovuti yake.
Mwanamke mmoja wa Florida, Marekani amemfikisha kizimbani 50 Cent kwa kuiweka video yake ya ngono kwenye tovuti yake.

Kwa mujibu wa nyaraka zilizowasilishwa mahakamani wiki hii, mwanamke aliyetambulika kwa jina la Lastonia Leviston alisema kuwa mwezi juni 2008 alirekodi video wakati akifanya mapenzi na mpenzi wake wa zamani lakini mpenzi wake huyo wa zamani alimuuzia 50 Cent video hiyo mwezi machi mwaka jana.

Taarifa zinasema kuwa 50 Cent aliinunua video hiyo na kuiweka kwenye tovuti yake katika njia zake za kuendeleza vita kati yake na rapa Rick Ross.

Taarifa zaidi zilisema kuwa Lastonia alikuwa ni mmoja wa wapenzi wa zamani wa Rick Ross.

50 Cent ambaye jina lake halisi ni Curtis James Jackson aliinunua video hiyo na kuifanyia marekebisho kwa kujifanya na yeye alikuwemo kwenye video hiyo akiwa amevaa wigi.

Video hiyo awali iliwekwa kwenye tovuti ya 50 Cent ya Thisis50.com kabla ya kusambaa kwenye tovuti kadhaa ikiwemo tovuti ya YouTube.

Video hiyo hadi sasa imeishaangaliwa na mamilioni ya watu duniani na Lastonia anamshitaki 50 Cent kwa kulitumia jina lake na video yake bila ya idhini yake.

Msemaji wa 50 Cent alipoulizwa kuhusiana na suala hilo alikataa kusema chochote.

source nifahamishe