Watengeneza filamu wa India wanawapima watu imani kwa kuahidi kutoa zawadi ya dola 10,000 kwa mtu yoyote atakayeweza kuangalia filamu mpya ya kutisha peke yake kwenye ukumbi wa sinema.
Nyota maarufu wa kutengeneza filamu za Kihindi Bollywood ameahidi kutoa zawadi ya dola 10,000 (Takribani Tsh. Milioni 13) kwa mtu yoyote atakayeweza kuangalia sinema mpya ya kutisha kuanzia mwanzo mpaka mwisho akiwa peke yake kwenye ukumbi wa sinema.
Filamu hiyo iliyotengenezwa na Ram Gopal Varma inayoitwa "Phoonk 2", ambayo ni sehemu ya pili ya filamu kama hiyo iliyotolewa mwaka jana, inaelezea mashetani wanavyozitesa familia.
"Mtu yoyote anayedai hawezi kutishika na sinema ya kutisha, atawekwa peke yake kwenye ukumbi wa sinema", alisema Varma alipokuwa akiitangaza filamu hiyo kwa waandishi wa habari mjini Mumbai.
Varma alisema kuwa mtu atakayejitokeza atawekewa nyaya za kupima mapigo ya moyo wake na pia atawekewa kamera ili kuhakikisha hafungi macho yake wakati wote wa filamu hiyo.
Matokeo ya vipimo vya mapigo ya moyo wake yataonyeshwa LIVE kwenye televisheni itakayowekwa nje ya ukumbi wa sinema. Mtu atakayefanikiwa kuangalia filamu hiyo toka mwanzo hadi mwisho atajipatia rupia za India 500,000.
Varma aliandaa shindano kama hilo kwenye filamu yake ya kwanza "Phoonk" ambapo ilitangazwa kuwa mtu aliyejitokeza aliweza kuangalia nusu saa tu kabla ya kukimbia.
Katika kumuonyesha Varma kuwa amechemsha mwanaume mmoja wa mji wa Bangalore alinunua tiketi za ukumbi mzima wa sinema na kuangalia filamu hiyo hiyo peke yake kuanzia mwanzo hadi mwisho huku mlinzi akiwa nje ya ukumbi.
source nifahamishe
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 comments:
Post a Comment