Waziri kizimbani kwa deni la Mil. 90

Friday, February 26, 2010 / Posted by ishak /


WAZIRI WA KILIMO, Chakula na Ushirika, Stephen Wasira, jana alipandishwa kizimbani katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu Dar es Salaam kwa tuhuma za kudaiwa shilingi milioni 90.
Kesi hiyo ilifikishwa na kusikilizwa mbele ya Hakimu Mkazi wa mahakama hiyo.

Ilidaiwa kuwa Wasira anadaiwa deni hilo na Andrew Ngai ambae ni Mkurugenzi wa Kampuni ya Cargo Building.

Shitaka la pili katika kesi hiyo ilidaiwa kuwa Wasira alimdhalilisha na kumsumbua mkurugenzi huyo.

Hakimu alipomtaka waziri huyo kujitetea mahakamani hapo alidai, alishangazwa na uwepo wa kesi hiyo, na kusema yeye ndio mwenye haki ya kumdai mkurugenzi huyo.

“Nashangaa kusikia mimi nashitakiwa wakati mimi ndio nimepata hasara ya vigae vyangu 600 vilivyokuwa kwenye kampuni yake kupotea”

Katika kesi hiyo ya madai yenye namba 24/2008, ilidaiwa na Wakili kuwa mwaka 1999 Waziri huyo aliagiza vigae 2,000 kutoka nchini Afrika Kusini na kumkabidhi Ngai anayeelezwa kuwa Mkurugenzi wa Kampuni ya Cargo Building amuhifadhie.

Wakili wa mshitakiwa aliiambaia mahakama kuwa, mteja wake alitumia vigae 1,400 na kubakiza 600 vilivyoelezwa kupotea na baadae Wasira kufungua kesi ya madai dhidi ya Ngai kutaka kulipwa shilingi milioni sita kama gharama za vigae 600 vilivyopotea lakini alishindwa katika kesi hiyo kesi.

Hivyo ilidaiwa kuwa baada ya kushindwa kwa kesi hiyo NGai alifungua kesi nyingine baada waziri huyo kushindwa mahakamani na kutaka kulipwa shilingi milioni 90 kama fidia ya usumbufu na kudhalilishwa kwa kampuni yake.

Hata hivyo Mahakamani iliahirisha kesi hiyo hadi Aprili 12 itakaporudi tena.


source nifahamishe