Member's Login Username Password Not a member? Sign Up Sign Out Afariki Kutokana na Moto wa Sigara

Monday, February 22, 2010 / Posted by ishak /


Mwanaume mmoja wa nchini Marekani amefariki dunia baada ya sigara aliyoiwasha kusababisha pombe kali aina ya Vodka aliyojimwagia kulipuka na kumuunguza.
Paul MacClymont, wa New Jersey nchini Marekani, aliungua vibaya na moto baada ya sigara aliyokuwa akivuta kuangukia kwenye nguo zake alizovaa ambazo alizimwagia pombe kali aina ya Vodka.

Paul mwenye umri wa miaka 40 alijibiringisha kwenye sakafu kwa nia ya kuuzima moto huo kabla ya kupoteza fahamu na kuzinduka baada ya masaa sita.

Huku akiwa na majeraha makubwa ya moto, Paul aliweza kuwapigia simu polisi ambao ilibidi wauvunje mlango wake ili kuweza kumfikia.

Paul aliungua asilimia 75 ya mwili wake na alifariki hospitalini siku ya ijumaa.

Kabla ya kufariki Paul aliwaambia polisi kuwa alikuwa akinywa Vodka siku nzima siku hiyo na kuna wakati pombe hiyo ilimwagikia kwenye suruali yake aliyovaa.

Wakati alipokuwa akiwasha sigara, sigara hiyo ilimuunguza mkono wake na yeye alilazimika kuiachia na ndipo ilipoangukia kwenye nguo alizovaa ambazo zilikuwa zimelowa pombe hiyo.

Moto ndipo ulipozuka na kuanza kumuunguza na kusababisha kifo chake.

source nifahamishe