Mahakamani kwa kudhalilisha

Wednesday, February 24, 2010 / Posted by ishak /

KIJANA Ali Othumani [26] amefiksihwa katika mahakama ya Mwanzo Kariakoo kwa tuhuma za kumdhalilisha Fatuma Bakari [22] kwa kumshika maungo ya mwilini pasipo ridhaa.
Ilidaiwa kuwa February 20, mwaka huu, majira ya mchana, huko maeneo ya Mtaa wa Mkunguni Kariakoo, mshitakiwa alianza kumdhalilisha malalmikaji kwa kumshika maungo yake ya mwilini pasipo ridhaa kutoka kwake.

Ilidaiwa mshitakiwa alishika matiti ya mlamikaji na kuchezea maungo yake ya mwilini pasipo ridhaa yake mbele ya hadhara ya watu na kumtia aibu kubwa.

Alipotakiwa kujibu tuhuma hizo mahakamani alipatwa na kigugumizi na kutaka hakimu amsamehe na hatorudia tena kitendo hicho.

Hakimu alimuuliza alikuwa anatambua kwamba wakati anafanya vitendo hivyo na huku mwenyewe akimkatalia alijua kama anamdhalisha?.

Alijibu kuwa hakutambua kwa kuwa alikuwa anajua kama anamtania .

Hakimu alimtaka Ali aende rumande kwa muda wa siku tatu ili aweze kupata adabu akirudi uraiani.

Hivyo amepelekwa rumande kwa muda wa siku tatu ili aweze kujirekebisha na atatolewa kwa dhamana siku hizo tatu zikikamika

Hakimu amefanya hivyo na amekataa kumpa dhamana ili kukomesha vitendo vya udhalilishaji kwa wanawake nchini

source nifahamishe