Madaktari wawili wa nchini Brazili walitwangana makonde kwa zaidi ya nusu saa badala ya kumhudumia mwanamke mjamzito aliyekuwa akiwasubiria wamalize kupigana ili wamzalishe.
Madaktari wawili wa nchini Brazili waliacha kazi ya kumzalisha mwanamke na kuanza kutwangana makonde mbele ya mwanamke mjamzito aliyetakiwa kuzalishwa kwa njia ya operesheni.
Mwanamke aliyejulikana kwa jina la Gislaine Santana, 32, aliingia kwenye leba na kusubiria kuzalishwa kwa njia ya operesheni wakati ngumi zilipozuka ghafla kati ya madaktari wawili ambao walitakiwa kumfanyia operesheni hiyo.
Kwa mujibu wa gazeti la Folha de Sao Paulo la Brazili, madaktari hao walitwangana makonde mazito na kugaragazana kwenye sakafu za wadi ya uzazi huku mwanamke huyo mjamzito akipiga kelele akitaka waache kupigana.
Daktari wa tatu alikuja dakika 90 baada ya tukio hilo na kumzalisha mwanamke huyo lakini mtoto wa kike aliyezaliwa alikuwa ameishafariki.
"Sitaki kusema chochote, lakini mpaka mke wangu anaingilia leba, mtoto wangu alikuwa bado yu hai na mwenye afya njema", alisema mume wa mwanamke huyo.
Mamlaka husika za nchini Brazili zimewafukuza kazi madaktari wote wawili waliodundana na wameanzisha uchunguzi kuhusiana na kifo cha mtoto huyo.
source nifahamishe
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 comments:
Post a Comment