Vijana Waliofanya Mapenzi na Mbuzi, Kuozeshwa Mbuzi

Saturday, February 27, 2010 / Posted by ishak /


Vijana wawili wa nchini Msumbiji ambao walikamatwa wakifanya mapenzi na mbuzi wamefikishwa mahakamani lakini mmiliki wa mbuzi huyo anaitaka mahakama iamuru vijana hao walipe mahari na waozeshwe mbuzi huyo.
Gazeti la serikali la nchini Msumbiji limeripoti kuwa vijana wawili wanaotuhumiwa kufanya mapenzi na mbuzi watapandishwa kizimbani kwa makosa ya jinai lakini mmiliki wa mbuzi huyo anataka taratibu za kimila zifanyike na wanaume hao waozeshwe mbuzi.

Vijana hao wawili ambao majina yao wala umri wao haukutajwa, walikamatwa na polisi wakifanya kitendo hicho katika mji wa Mbucuta uliopo ukanda wa kati wa Msumbiji.

"Mmoja wa vijana hao alikuwa uchi akikishikilia kichwa cha mbuzi wakati kijana mwingine alikuwa akifanya mapenzi na mbuzi huyo", alisema mmoja wa mashuhuda wa tukio hilo, Mario Creva alipokuwa akiongea na radio Msumbiji.

Mwendesha mashtaka wa serikali amesema kuwa vijana hao wawili watapandishwa kizimbani hivi karibuni.

Lakini mmiliki wa mbuzi huyo anaweza akafungua kesi nyingine akitaka vijana hao waozeshwe mbuzi huyo.

Mmiliki wa mbuzi huyo anataka vijana hao walipe fidia kwa uharibifu wao na kisha waanze taratibu za kitamaduni kwa kulipa mahari kabla ya kuozeshwa mbuzi huyo.source nifahamishe