Mwanamke Aliyesingizia Kubakwa Atupwa Jela

Wednesday, February 24, 2010 / Posted by ishak /


Mwanamke wa nchini Marekani aliyemsingizia mwanaume asiye na hatia kuwa amembaka na kusababisha mwanaume huyo atupwe jela, amehukumiwa kwenda jela baada ya kutubu kanisani kuwa aliongopa kubakwa na mwanaume huyo.
Biurny Peguero mwenye umri wa miaka 27 mkazi wa jiji la New York nchini Marekani amehukumiwa kwenda jela kati ya mwaka mmoja na miaka mitatu baada ya kukiri kumsingizia mwanaume asiye na hatia kuwa amembaka.

Mwaka 2005, Biurny alimsingizia mwanaume huyo kuwa alimtishia na kisu kabla ya kumbaka. Mwanaume huyo alihukumiwa kwenda jela miaka minne.

Mwaka jana Biurny alienda kutubu madhambi yake kanisani na kukiri mbele ya mchungaji kuwa alimsingizia mwanaume asiye na hatia kuwa amembaka.

Hatua hiyo ilisababisha polisi wapewe taarifa ambapo mwanaume huyo aliachiliwa huru muda mfupi baadae.

Akisomewa hukumu yake, Biurny alihukumiwa kwenda jela kutumikia kifungo cha kati ya mwaka mmoja na miaka mitatu.

source nifahamishe