Kufanya Operesheni Ili Afanane na Supastaa wa Marekani

Sunday, January 31, 2010 / Posted by ishak /


Ili kumfanya mpenzi wake wa zamani amrudie tena, mwanamke mmoja wa nchini China anafanya operesheni ya kuubadilisha mwili wake ili afanane na nyota wa Marekani, Jessica Alba.
Mwanamke mwenye umri wa miaka 21 aliyejitambulisha kwa jina la Xiaoqing wa nchini China ameamua kufanya operesheni ya kuubadilisha mwili wake ili afananane na mcheza sinema wa Marekani, Jessica Alba.

Mwanamke huyo aliliambia gazeti la Shanghai Daily kuwa ameishakutana na madaktari wa operesheni za urembo wa mjini Shanghai ambao wamemuahidi watamfanyia operesheni hiyo bure.

Xiaoqing aliliambia gazeti hilo kuwa atafanya operesheni za kuubadilisha mwili wake ili afanane na Jessica Alba kwakuwa mpenzi wake wa zamani anampenda sana mcheza sinema huyo hivyo anaamini kuwa atakapofanana naye basi mpenzi wake atamrudia.

Afisa wa hospitali ya Shanghai Time Plastic Surgery Hospital, ambayo Xiaoqing atafanyiwa operesheni zake alisema kuwa Xiaoqing atafanyiwa bure operesheni za kurekebisha kope na nyusi za macho yake pamoja na operesheni ya pua yake ili aweze kufanana na Jessica Alba ambaye alitamba kwenye "Sin City" na "Fantastic Four".

"Hakuna wasiwasi wa malipo, operesheni inawezekana kufanyika", alisema afisa huyo na kuongeza "Inabidi afahamu kuwa hataweza kuirudia sura yake ya zamani baada ya operesheni".

Xiaoqing alisema kuwa mpenzi wake huyo wa zamani anampenda sana Jessica Alba kiasi cha kwamba kwenye ukuta wa chumba chake ameweka picha yake kubwa na hata kwenye simu yake kuna picha za msanii huyo maarufu wa Marekani.

Xiaoqing aliongeza kuwa mpenzi wake huyo alikuwa akimlazimisha ajipodoe kama Alba na alimnunulia wigi ambalo alimtaka alivae wakati wote. Xiaoqing alisema kuwa uhusiano wao ulivunjika baada ya kuamua kulivua wigi hilo na kulitupa.

"Nampenda sana ndio maana nafanya hivi... sitaki kumpoteza ", alimalizia kusema Xiaoqing.

source nifahamishe

0 comments:

Post a Comment