Daktari mbaroni kwa kudaiwa kubaka mgonjwa

Tuesday, February 02, 2010 / Posted by ishak /

DAKTARI wa Hospitali ya Marie Stoppers iliyopo Mwenge, jijini Dar es Salaam, Paul Andrew ametiwa mbaroni kwa tuhuma za kudaiwa kumbaka mgonjwa aliyefika hospitalini hapo wakati akimpatia matibabu
Ilidaiwa kuwa mgonjwa huyo alifika hospitalini juzi, majira ya jioni kwa lengo la kupatiwa matibabu wakati alikuwa akisumbuliwa na ugonjwa wa tumbo na alifika kwa ajili apatiwe uchunguzi wa kina ili tatizo lake liweze kugundulika.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kinondoni, Elias Kalinga alithibitisha kuwa mgonjwa huyo alifika hospitalini hapo kwa ajili ya kufanyiwa uchunguzi wa kina wa tumbo llilokuwa likimsumbua.

Alisema alipofika hapo alikutana na daktari huyo aliyetambulika kama Dk. Andrew na alimwandikia afanyiwe kipimo cha Utra Sound ili aweze kugundulika tatizo lake.

Kalinga alisema alithibitisha tukio hilo kwa mujibu wa maelezo ya mgonjwa

Alisema baada ya mgonjwa huyo kuingia katika chumba cha kufanyiwa kipimo hicho ndipo daktari huyo alimpa kitu kilichomfanya alale kwa muda na nguvu ya dawa ilipokwisha alishtuka na kumkuta daktari huyo akiendelea kumbaka.

Alisema mgonjwa huyo alipozinduka na kujikuta akibakwa na daktari huyo alijinasua na alitoka nje na kukimbilia Kituo cha Polisi Mabatini kilichopo Kijitonyama na kufungua jalada lenye namba RB/KJN/123/552/10.

Alisema mgonjwa huyo aliongozana na askari wa kituo hicho hadi hospitalini na kumkamata mtuhumiwa aliyekuwa bado yupo eneo hilo.

Kamanda Kalinga alizidi kutoa maelezo hayo kuwa, kutokana na maelezod ya utatanishi wa mgonjwa huyo ilibidi jeshi hilo apelekwe kufanyiwa vipimo Hospitali ya Taifa ya Muhimbili ili kubaini kama kweli alifanyiwa unyama huo.

Baada ya vipimo kufanyika iligundulika alifanywa na mtuhumiwa anashikiliwa na polisi

source nifahamishe