Binti mwenye umri wa miaka 12 wa nchini Saudi Arabia ambaye alimkimbia mumewe mwenye umri wa miaka 80 baada ya kufungishwa ndoa kinguvu na baba yake, amekubali kurudi kwa mumewe na kuyaondoa madai ya talaka aliyofungua mahakamani.
Msichana mwenye umri wa miaka 12 wa nchini Saudi Arabia ambaye kwa kushirikiana na mama yake alifungua kesi mahakamani kudai talaka toka kwa mumewe mwenye umri wa miaka 80 ameamua kuyaondoa madai yake ya talaka na kurudi kwa mumewe.
Msichana huyo aliozeshwa kinguvu na baba yake ambaye alichukua mahari ya dola 22,670 toka kwa babu huyo.
Binti huyo ambaye jina lake limewekwa kapuni, alikuwa akiishi na baba yake baada ya ndoa ya baba yake na mama yake kuvunjika.
Binti huyo na mama yake waliifuta kesi ya madai ya talaka waliyoifungua katika kitongoji cha Buraidah katika mji wa Al-Qasim.
"Nimeikubali ndoa iliyofungwa na sina kipingamizi chochote", alisikika akisema binti huyo na kuongeza "Nafanya hivi kwaajili ya heshima ya baba yangu na kumtimizia ndoto yake".
Bila ya kueleza sababu za kubadilisha uamuzi wake ghafla, binti huyo aliiambia mahakama kuwa ndoa hiyo ilifungwa kwa hiari yake.
Ndoa ya binti huyo na babu mwenye umri wa miaka 80 ilizua mtafaruku mkubwa sana duniani baada ya mama wa binti huyo kufungua kesi mahakamani kuipinga ndoa hiyo huku akidai binti yake amebakwa.
Wakati taasisi za kutetea haki za watoto zikijiandaa kumtetea mahakamani, binti huyo amezivunja moyo taasisi hizo na kukubali kurudi kwa mumewe.
source nifahamishe
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 comments:
Post a Comment