Kibonge wa Dunia Apungua Kilo 127,Lakini Bado Anaongoza

Tuesday, February 02, 2010 / Posted by ishak /


Mtu mnene kuliko wote duniani amepungua kilo 127 baada ya kufanyiwa operesheni ya kuokoa maisha yake lakini bado ameendelea kutambulika kama mtu mnene kuliko wote duniani kwa kilo zake 311 zilizobaki.
Baada ya kupungua kilo 127, Mtu mnene kuliko wote duniani, Muingereza Paul Mason hivi sasa ana uzito wa kilo 311 na ameendelea kushikilia taji la unene duniani.

Mason mwenye umri wa miaka 48, alitumia mwisho wa wiki kwenye kitanda cha kitengo maalumu cha hospitali baada ya kufanyiwa operesheni kubwa ya kumzuia kuendelea kunenepa na kuondolewa kwa mafuta kwenye tumbo lake.

Katika operesheni hiyo tumbo la Mason lilipasuliwa na kutengenezwa kisehemu kidogo kama pochi kwaajili ya kuhifadhi chakula chake.

Kwa maana hiyo chakula chake chote hivi sasa kitaenda kwenye hicho kipochi na hivyo kumfanya awe anakula kiasi kidogo sana cha chakula.

Wiki iliyopita madaktari walimuingiza Mason kwenye diet ya nguvu ya kuupunguza unene wake ili aweze kuwa fiti kwaajili ya operesheni.

Mason ameelezea nia yake ya kupunguza uzito wake zaidi ili aweze kuendesha gari.

Mwaka 2002 kutokana na unene wa Mason, Zimamoto iliwabidi waubomoe ukuta wa chumba chake na kisha kutumia forklift ili kuweza kumbeba na kumwingiza kwenye ambulansi kumwahisha hospitali kwaajili ya operesheni ya hernia.

Wakati huo alikuwa na uzito wa kilo 355, aliwaambia madaktari kuwa anataka kupunguza uzito wake lakini alianza kula sana ili kuvunja rekodi ya dunia awe mtu mnene kuliko wote duniani.

Hatimaye mwaka jana alifanikiwa kuvunja rekodi hiyo kwa kufikisha uzito wa kilo 444 na kumfunika kibonge wa dunia wa wakati huo toka Mexico, Manuel Uribe ambaye aliamua kupunguza uzito wake ili aweze kumuoa mpenzi wake.

source nifahamishe

0 comments:

Post a Comment