Hausigeli aanguka kutoka ghorofani na kufa

Wednesday, February 03, 2010 / Posted by ishak /

MSICHANA wa kazi za ndani aliyefahamika kwa jina moja la Modiwa anayekadiriwa kuwa na umri kati ya miaka 20 na 25, mkazi wa Kariakoo Mtaa wa Livingstone amekufa baada ya kuteleza kutoka kwenye ghorofani.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Ilala, Faustine Shilogile amesema kuwa, ajali hiyo imetokea jana saa 3 usiku, huko Kariakoo Mtaa wa Livingstone.

Maelezo ya Shilogile yalisema kuwa, msichana huyo alikuwa ni mfanyakazi nyumbani kwa Hassan.

Alisema kuwa msichana huyo aliteleza kutoka ghorofa ya nne kisha kuanguka chini na kufa papo hapo.

Maiti imehifadhiwa chumba cha maiti Hospitali ya Taifa ya Muhimbili na Polisi wanaendelea na uchunguzi zaidi kuhusiana na tukio hilo..

source nifahamishe