Afikishwa kortini kwa kuua wanawe

Friday, February 05, 2010 / Posted by ishak /

MOSES CHIPAMA [45] anayedaiwa kuwaua watoto wake wawili katika mazingira ya kutatanisha jana alifikishwa katika Mahakama ya Wilaya ya Temeke kujibu shitaka hilo la mauaji.
Shata hilo lilifikishwa mbele ya Hakimu Mkazi, Rose Kangwa, wakati upande wa mashitaka ulikuwa ukiongozwa na Inspekta Dustan Kombe.

Kombe alidai kuwa mshtakiwa anakabiliwa na mashitaka mawili ya mauaji ya watoto wake.

Katika shitaka la kwanza mshtakiwa alikamatwa Januari 25, mwaka huu, majira ya saa 5:55 usiku eneo la Tuangoma kwa Saku baada ya kumuua mtoto wake, Patrick Moses (16), aliyekuwa akisoma darasa la saba Shule ya Msingi Tuangoma.

Katika shitaka la pili, ilidaiwa kuwa mshtakiwa huyo alimuua mtoto wake mwingine, Sety Moses (12), aliyekuwa akisoma darasa la nne katika Shule ya Msingi ya Olympio.

Hata hivyo mshitakiwa alirudishwa rumande kwa kuwa hakutakiwa kujibu chochote mahakamani hapo kwa kuwa mahakama hiyo haina mamlaka ya kusikiliza kesi hiyo.

Hakimu aliamuru arudishwe rumande na kusubiri tarawtibu za kimahakama zifanyike na atakwenda kujibu shitaka hilo mahakama kuu, Kesi hiyo itarudishwa tena mahakamani hapo Februari 18, mwaka huu.

Katika hali ya kushangaza mshitakiwa huyo alianza kuwarushia mawe waandishi wa habari waliokuwa ndani ya mahakama kusikiliza shauri hilo huku akiwarushia viatu kwa kukataa kuandikwa na na kupigwa picha.

Alipoona viatu vyote viwili alivyovaa viliisha alivua fulana aliyovaa na ulijifunika sura ili wanahabari wasiweze kupata sura ili wasiweze kuianika magazetini.

Kutokana na fujo zake hizo maaskari magereza walilazimika kumtuliza mshitakiwa huyo kwa virungu na kuacha kuwatukana matusi wanahabari.


source nifahamishe