Wanne wa familia moja wateketea kwa moto wa jenereta

Thursday, February 04, 2010 / Posted by ishak /

WATU wanne wa familia moja wamekufa kwa moto baada ya jenereta lililokuwa limefungiwa katika moja ya chumba ndani ya nyumba hiyo kupasuka na kuwaka moto
Tukio hilo la kusikitisha limetokea usiku wa kuamka leo, huko maeneo ya Kibwenzini Zanzibar wakati watu hao wakiwa wamelala ndani humo.

Ilidaiwa kuwa jenereta hilo liliripuka majira ya saa 11 za alfajiri na kuzua moto uliosababisha vifo hivyo.

Ilidaiwa kuwa familia hiyo ilinunua jenereta hilo kwa ajili ya matumizi ya nyumbani kutokana na kukosekana kwa umeme visiwani Zanzibar.

Katika ajali hiyo waliopoteza maisha walitajwa kuwa ni Safia Shabani, Ahmed Shaban na mtoto ambaye hakuweza kupatikana jina lake, akiwemo na msichana wa kazi Sikudhani Nasorro.

Hadi habari hii inarushwa hewani, kamanda wa Polisi wa wilaya husika hakuweza kupatikana kuongelea juu ya tukio hilo juhudi zaidi zinafanyika ili kuweza kupata maelezo yake.

source nifahamishe