Mashine ya Kuwatawadhisha Waislamu Yavumbuliwa nchini Malaysia

Tuesday, February 02, 2010 / Posted by ishak /


Kampuni moja nchini Malaysia imevumbua mashine ambayo itakuwa ikiwatawadhisha waislamu kabla ya sala ambayo inatumia maji kiasi cha lita 1.3 tu.
Mshine hiyo imevumbuliwa na kampuni ya nchini Malaysia ya AACE Technologies kwaajili ya kuwasaidia waislamu kutia udhu bila kutumia maji mengi.

Mashine hiyo inatumia misingi yote ya sheria za kiislamu katika kutawadha na imepitishwa na serikali ya Malaysia kutumia kuwatawadhisha watu.

Mashine hiyo yenye urefu wa mita 1.65 inayojulikana kama "The Auto Wudu Washer" inatumia mabomba yenye sensor kumtawadhisha mtu mmoja katika hali ya kusimama kwa kutumia lita 1.3 tu.

Mashine hiyo itasaidia kupunguza upotevu wa maji wakati wa kutawadha ambapo kawaida bomba huachwa wazi muda wote wakati wa kutia udhu, alisema mwenyekiti wa AACE, Anthony Gomez.

Kuna waislamu zaidi ya bilioni 1.7 duniani ambapo asilimia kubwa ya waislamu wapo Afrika na mashariki ya kati ambako kuna uhaba wa maji.

Mashine hiyo imepokelewa vizuri katika nchi tajiri za kiarabu ambazo zimeelezea mpango wa kuzinunua mashine hizo.

Mashine hizo mbali ya kumtawadhisha mtu, humwezesha mtu anayetawadha kusikiliza quran huku akitawadhishwa.

"Wakati wa Hija, watu milioni 2 hutumia lita milioni 50 za maji kwa siku moja kwaajili ya udhu, kwa kutumia mashine hizi wangeweza kuokoa lita milioni 40 kwa siku", alisema Gomez.

Dubai ina mpango wa kunua mashine hizo na kuzitumia kwenye viwanja vyake vya ndege kwaajili ya misikiti iliyopo kwenye viwanja hivyo.

source nifahamishe

0 comments:

Post a Comment