Uvaaji Wako wa Suruali Hudhihirisha Umri Wako

Tuesday, February 02, 2010 / Posted by ishak /


Kwa mujibu wa matokeo ya utafiti uliofanyika hivi karibuni, uvaaji wa suruali wa mwanaume huendana na umri alio nao, wakati vijana wengi hushusha suruali zao chini ya makalio wanaume wanaoanza kuzeeka huzipandisha suruali zao juu ya kiuno.
Utafiti uliofanywa na watafiti wa Uingereza umedhihirisha kuwa kuna uhusiano wa uvaaji wa suruali wa mwanaume na umri wake.

Paul Baldwin, mkurugenzi wa nguo za kiume katika duka kubwa la nguo na vipodozi la Debenhams, la nchini Uingereza ambalo liliendesha utafiti huo, alisema kuwa kuna uhusiano wa mkubwa kati ya uvaaji wa suruali wa mwanaume na umri wake.

Watoto chini ya miaka 12 kawaida huvaa suruali zao kwenye usawa wa kiuno kwakuwa kwa umri huo hununuliwa nguo na wazazi wao na wakati mwingine kuvalishwa na wazazi wao.

Wanapofikisha umri wa kati ya miaka 16 na 26 huanza kuwaiga waimbaji wa Hip Hop wa Marekani na kuanza kuvaa suruali zao chini ya makalio. (kata K).

Mwanaume anapokuwa na umri kati ya miaka 27 na 39 huanza kuvaa suruali kwa jinsi inavyotakiwa iwe usawa wa kiuno. Miongoni mwa sababu zinachongia kumfanya mwanaume aanze kubadilika ni masuala ya kazi au kuoa.

Mwanaume anapofikisha umri wa miaka 45, kama vile dalili ya kuanza kwa uzee, suruali nayo huanza kupanda juu na kuvaliwa nchi mbili juu ya kiuno. Suruali huendelea kupandishwa juu ya kiuno na kufikia inchi 5 mwanaume anapofikisha umri wa miaka 57.

Kuanzia umri wa miaka 65, kiuno cha mwanaume huanza kunywea ndani na hivyo kuifanya suruali ianze kushushwa chini taratibu hadi kufikia usawa wa inchi moja tu juu ya kiuno mwanaume anapofikisha umri wa miaka 75.

Utafiti huu ulifanywa kwa kushirikisha jumla ya wanaume 1,000.


source nifahamishe

0 comments:

Post a Comment