Mwanamke Ajilipua nchini Iraq na Kuua Watu 54

Tuesday, February 02, 2010 / Posted by ishak /


Mwanamke aliyekuwa ameficha mabomu ndani ya nguo zake, amejilipua katika mkusanyiko wa waumini wa kiislamu wa dhehebu la shia nchini Iraq na kupelekea vifo vya watu 54 na wengine 117 kujeruhiwa.
Mwanamke huyo akiwa ameyaficha mabomu kwenye nguo zake alifanikiwa kuingia kwenye hema la wanawake na watoto na kujilipua.

Jumla ya watu 54 wameishafariki kutokana na shambulio hilo na wengine 117 wamejeruhiwa.

Tukio hilo lilitokea wakati waumini wa Shia walipoweka kambi ya muda ya mapumziko kabla ya kuendelea na safari ya kuelekea mji wa Karbala uliopo kilomita 110 toka Baghdad.

Asilimia kubwa ya watu waliofariki na waliojeruhiwa ni akina mama na watoto ambao walikuwa kwenye hema moja na mwanamke huyo.

Maelfu ya waumini wa Shia walikuwa wakiandamana wakitembea kuelekea kwenye mji wa Karbala kwaajili ya ibada za Shia za kuomboleza kifo cha mjukuu wa mtume Muhammad (s.a.w), Hussein ambaye alifariki kwenye karne ya 7 katika vita vya Karbala.

Maelfu ya waumini wa Shia toka nchi mbali mbali duniani walijumuika katika ibada hiyo.

Tukio la kujilipua la mwanamke huyo limetokea huku walinzi 30,000 wa Iraq wakishiriki kuimarisha usalama kwenye ibada hizo.

Hata hivyo waumini wa Sunni wanye kupingana na Shia wamekuwa wakifanikiwa kujipenyeza na kusabababisha maafa kila mwaka wakati wa mkusanyiko wa ibada hizo.

source nifahamishe