Pinda aguswa na sakata la Jerry

Friday, February 05, 2010 / Posted by ishak /


WAZIRI MKUU Mizengo Pinda, ameliagiza Jeshi la polisi nchini kufanya uchunguzi haraka iwezekanavyo ili suala hilo liweze kujulikana kama ni la fufikishwa mahakamani ama la ili haki iweze kutendeka kwa kuwa suala hilo limeigusa jamii iliyokubwa nchini
Pinda amemuagiza Mkuu wa Jeshi hilo IGP Said Mwema na Waziri wa Mambo ya Ndani, Lawrence Masha kufanya uchunguzi wa kina bila kuvihusisha vyombo vya habari ili kuweza kumaliza sakata hilo.

Waziri Pinda alitoa agizo hilo jana wakati alipokuwa akijibu maswali ya papo kwa papo bungeni Dodoma.

Pinda ambaye ni kiongozi wa kwanza wa ngazi za juu wa serikali kuingilia kati ametaka suala hilo lishughulikiwe mara moja tuhuma za mwanahabari huyo ambalo kwa sasa limekuwa gumzo la jiji.

Agizo la Waziri Mkuu lilitokana na swali la Kiongozi wa Kambi ya Upinzani Bungeni na Mbunge wa Wawi, Hamad Rashid Mohamed (CUF), aliyehoji jitihada zinazofanywa na serikali katika kushughulikia suala hilo.

Katika swali lake la msingi, Hamad Rashid alisema waandishi wengi duniani wanapofuatilia mambo mazito, hupatwa na misukusosuko mikubwa na kuhoji kama yaliyompata Muro ni mojawapo ya misukosuko ya aina hiyo.

Akijibu swali hilo, Pinda alisema tayari amekwishazungumza na Masha na IGP Mwema ambao wameahidi kulifuatilia jambo hilo kwa haraka na binafsi asingependa jambo hilo kuendelea kuleta utata kutokana na kuwepo na kauli nyingi za watu mbalimbali kuhusu suala husika.

Pia alisema “Mimi pia sipendi suala hili lichukue muda mrefu maana linaweza kuleta hisia tofauti miongoni mwa jamii,” alisema Pinda.

Alisema kila binadamu anao upungufu wake, hivyo kuna uwezekano wa tuhuma dhidi ya Muro zikawa za kweli au la kwani pande zote mbili, akiwemo Muro na polisi wamekuwa wakikimbilia katika vyombo vya habari na kutoa taarifa zinazotatanisha.

source nifahamishe

0 comments:

Post a Comment